A song made by Mwl. Imani Nyingi
A song made by Mwl. Imani Nyingi
WATU WAWILI
Watu wawili walipanda Hekaluni, kwenda kusali na kuungama dhambi zao kwa Mungu
Wa kwanza alikuwa Mfarisayo
Na wapili alikuwa Mtoza ushuru, wawili hawa walipanda hekaluni kusali
Yule mfarisayo alisimama...
Akaomba moyoni mwaka huku akisemaaa hivi..
"Eeh Mungu nashukuru kwa kuwa mimi sio kama watu wengine..
Wale wanyang'anyi, wadharimu, wazinzi wala mimi sio kama huyu, mtoza ushuru..
Mimi nafunga mara mbili kwa juma, natoa zaka katika mapato yangu uuu mapato yoteeeee!!"
Lakini mtoza ushuru alisimama mbali
Wala hakuthubutu kuinua macho yake mbinguni,
Yeye alisema.....
"Eeeh Mungu uniwie radhi mimi, mwenye dhambiiii Bwana.. .
Eeeh Mungu uniwie radhi mimi, mwenye dhambiiii Bwana.. "
Bwana anasema, yule mtoza ushuru amehesabiwa haki mbele za Mungu
Bwana anasema, yule mtoza ushuru amehesabiwa haki mbele za Mungu
Unapomweleza Mungu shida zako, jishushe kwake, ndugu umwelezapo Mungu shida jinyenyekeze
Bwana anasema, yule mtoza ushuru amehesabiwa haki mbele za Mungu
Bwana anasema, yule mtoza ushuru amehesabiwa haki mbele za Mungu
Usiwe na kiburi cha uzima maisha haya, kuwaona wengine ni wadhambi na wewe u mwema
Bwana anasema, yule mtoza ushuru amehesabiwa haki mbele za Mungu
Bwana anasema, yule mtoza ushuru amehesabiwa haki mbele za Mungu
Usijione wewe ndiwe bora kuliko wengine, Mungu huangalia moyo wenye kupondeka!!
Bwana anasema, yule mtoza ushuru amehesabiwa haki mbele za Mungu
Bwana anasema, yule mtoza ushuru amehesabiwa haki mbele za Mungu
Yule ajikwezaye
hakika atashushwa
Na yule ajishushaye
Huyo atakwezwa
Yule ajikwezaye baba aaah
hakika atashushwa
Na yule ajishushaye
Huyo atakwezwa.... acha!!
Acha mara moja
Acha kujikweza, baba Mungu mwenyewe, atakukweza kwa wakati wake unaofaa,
Acha kujikweza, baba Mungu mwenyewe atakukweza kwa wakati unaofaa
Yule ajikwezaye
hakika atashushwa
Na yule ajishushaye
Huyo atakwezwa..... Acha..